Imeripotiwa kuwa Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Michael Sarpong ameingia katika hatua nyingine ya mgogoro na Uongozi wa klabu ya Young Africans, baada ya kusamehewa kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Sarpong ambaye aliamuriwa kurejea kambini majuma mawili yaliyopita, anatajwa kuwa kwenye mvutano na viongozi wa klabu hiyo ya Jangwani, kufuatia mpango wa kuvunjiwa mkataba wake, ili aondoke na nafasi yake kujazwa na mchezaji mwingine wa kimataifa.

Kwa sasa nyota huyo hayupo kwenye mipango ya msimu ujao ya Kocha Nabi na ameambiwa nia ya klabu hiyo ya kuvunja mkataba wake.

Inadaiwa kuwa Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Ryon Sports ya Rwanda ameuambia Uongozi wa klabu ya Young Africans kuwa kama wanataka kuvunja mkataba wake uliobaki lazima wamlipe dola 31,000 (zaidi ya milioni 71 za Kitanzania) na si vinginevyo.

Sarpong mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Young Africans Agosti 2020 kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru akitokea Rwanda.

Ilanfya: Narudi Simba SC kupambana
Real Madrid kumuweka sokoni Eden Hazard