Chama cha soka nchini Saudi Arabia (SAUDI ARABIA FOOTBALL FEDERATION) kimejipanga kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2034.  taarifa za ndani zinasema chama hicho kwa kushirikiana na serikali  wameshaandaa viwanja 15 katika miji 5 ambavyo vyote vimekubalika na FIFA na vitatumika katika michuano hiyo.

Saudi Arabia inakuwa nchi ya pili ya kiarabu kuandaa michuano hiyo baada ya Qatar iliyoandaa michuano hiyo mwaka 2022. Awali Saudi Arabia ilitaka kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2030 lakini ilijiondoa katika kinyang’anyiro hicho na nchi za Hispania Ureno na Morroco zikaungana kuandaa kombe la dunia  kwa mwaka 2030.

Saudi Arabia ilifanikiwa kupata kibali cha kuandaa michuano ya mwaka 2034 baada ya kupata ushindi mbele ya chama cha soka  Asia na muunganiko wa nchi za New zealand na Australia. Nchi hiyo ilijisajili rasmi FIFA mwaka 1956 na imefanikiwa kushiriki michuano ya kombe la dunia mara 6 ikifanikiwa kuingia hatua ya 16 bora mara moja.

 

Hawa hapa wanaowania Tuzo za TFF Usiku wa leo
TLS isimamie haki, amani kuchochea maendeleo: Dkt. Biteko