Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji.
Kampuni hiyo inayomiliki viwanda mbalimbali nchini Saudi Arabia inajishughulisha na uzalishaji wa pembejeo za Killimo hususan, mbolea za kupandia na kukuzia mimea pamoja na dawa (pesticides) aina ya ‘phosphorus, nitrogen, potassium na sulfur’.
Ujumbe wa wawekezaji hao umeongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia Mhe. Ali Mwadini na umtembelea Mikoa ya Mtwara, Lindi na Dodoma na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mikoa hiyo.
Wawekezaji hao wamemuhakikishia Mhe. Waziri Mulamula nia yao ya kuja kuwekeza Tanzania na kutaja maeneo ambayo ni kipaumbele chao kuwa ni madini, biashara, kilimo na mifugo