Saudi Arabia imesema kuwa mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi alikufa baada ya kupigana kwenye ubalozi wake mdogo wa mjini Istanbul, Uturuki. Uchunguzi bado unaendelea na hadi sasa raia 18 wa Saudi wamekamatwa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari vya serikali nchini Saudi Arabia imesema kuwa, mshauri wa mahakama ya Saudi Arabia, Saud al-Qahtani na naibu Mkuu wa idara ya upelelezi, Ahmed Asiri wamefukuzwa kazi. Kabla ya Saudi Arabia kutoa taarifa hiyo mapema leo.

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema anaweza kuiwekea vikwazo Saudi Arabia lakini wakati huo huo amesisitiza umuhimu wa uhusiano wa nchi hizo mbili. ambapo amesema kuwa maelezo yaliyotolewa na Saudi Arabia ni ya kuaminika.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la Saudi Arabia (SPA) mabishano kati ya Jamal Khashoggi na watu aliokutana nao kwenye ubalozi huo mdogo yaligeuka na kuanza kurushiana Makonde ugomvi ambao ulisababisha kifo chake.

Aidha, Saudi Arabia haikutoa ushahidi wa kuunga mkono maelezo yake kuhusu hali halisi ilivyokua na haijulikani kama washirika wake wa Magharibi wataridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Saudi Arabia.

Mkasa wa kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari ulisababisha kilio kutoka kwa jamii ya kimataifa na pia kuleta hali ya mvutano kati ya Saudia na nchi za magharibi.

Hata hivyo, Khashoggi, ambaye alikuwa mkosoaji mkuu wa sera ya mwana mfalme Mohammed bin Salman, alitoweka baada ya kuingia ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul mnamo tarehe 2 mwezi huu kwa ajili ya kupata hati ambayo ingemuwezesha kufunga ndoa na mchumba wake wa Kituruki.

 

Umoja wa Mataifa watangaza vita dhidi ya upimaji ubikira
Msako wawatia mbaroni raia wawili wa kigeni Dar