Ndege za kivita za majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia zimedaiwa kuushambulia kwa makombora ubalozi wa Iran nchini Yemen.

Kituo cha Utangazaji cha Iran cha Irinn kimeeleza kuwa makombora yaliyorushwa na ndege hizo za kivita yalitua katika ubalozi wa nchi hiyo ulioko jijini Sanaa na kusababisha uharibifu mkubwa wa majengo na kuwajeruhi walinzi kadhaa.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Hossein Jaberi Ansari alinukuliwa na kituo hicho cha utangazaji akieleza kuwa shambulizi hilo la makusudi limevunja sheria za kimataifa.

“Kitendo hiki cha makusudi kilichofanywa na Serikali ya Saudi Arabia ni uvunjifu wa sheria zote za kimataifa na makubaliano kuhusu kulinda maeneo ya kidiplomasia kwa namna yoyote,” Ansari alikaririwa.

Kumekuwa na taharuki kati ya nchi hizo mbili baada ya Saudi Arabia kumuua mhubiri maarufu wa Ki-Shia wa Iran baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya ugaidi. Wananchi wa Ki-Shia waliandamana nchini Iran na kuchoma ubalozi wa Saudi Arabia nchini humo.

 

 

Wajifungia Kuisuka Upya Chadema
Sababu za Wasanii Kukataa Kulipwa Kwa Nyimbo zao Kuchezwa Redioni/TV zawekwa wazi