Kundi la wanamuziki wa Kenya la sauti Sol limeweka rekodi mchini humo kwa kuwa wasanii wa kwanza nchini Kenya kufikisha idadi ya wafuasi ‘followers’ milioni moja katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
Kwa hapa Tanzania ni jambo la kawaida sana kwa mwanamuziki kuwa na wafuasi milioni moja na hata zaidi mitandaoni kwakuwa watanzania wengi wameweka mbele maswala ya mitandao ya kijamii na hasa Instagram, na huwafuatilia wasanii wanaowapenda kwenye kurasa zao za mitandao lakini kwa nchi jirani za Africa Mashariki ni tofauti kidogo.
Baada ya kufanikiwa kuongeza idadi hiyo, wasanii hao kupitia mtandao wa Twitter wamesherekea kwa kuandika, “Habari za asubuhi kwa sasa sisi ndio wanamuziki wa kwanza wa Kenya kufikisha wafuasi milioni moja kwenye Instagram’’.
-
Kanye West awa mpole, aomba kukutana na Jay Z wamalize ugomvi wao
-
Kundi la ‘Camp Mulla’ kurudi na Album mpya
-
Video: Young D kaja na ‘Kiutani utani’
Kwa sasa sauti Sol waliotamba na ngoma kadha kama Kuliko jana,Sura yako na Nishike kwa sasa wapo kwenye ziara ya show zao nchini Ujerumani na Ubelgiji.
Kundi la Sauti Sol linaundwa na wasanii; Bien-Aimé Baraza , Polycarp Otieno, Delvin Mudigi na Willis Austin Chimano.