Mwanaharakati Mange kimambi ametoboa siri kilichomfanya Wema Sepetu akwae taji la Umiss Tanzania 2006 na kumpiku Jokate Mwagelo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Mange Kimambi kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram amesema kipindi cha mashindano ya Umiss Tanzania 2006, alimpa majibu Wema Sepetu akariri ili aweze kujibu vizuri na kutwaa taji hilo na kusema bila kufanya hivyo asingeweza kumshinda mpinzani wake ambaye kwa sasa ni Mhe. Jokate.

”Kama isingekuwa shobo zangu hilo taji la miss tanzania usingelipata kabisa…i really made literally kama usingemshinda jokate kwenye maswali basi wala usingetwaa taji..maswali ambayo mimi nafaraja kota tulikalisha matako yetu chini tukasearch na kuyatafakari , tukakuandikia majibu theni nikakuletea majibu na kukremu” amesema Mange Kimambi katika ukurasa wake wa Instagram.

Kumetokea malumbano makumbwa katika mtandao wa Instagram mara baada ya kutokea mtafaruku mkubwa baada ya kuvuja kwa clip ya Hamisa akiongea na mganga wa kienyeji kuwa kuna mambo anataka amsaidie juu ya penzi lake na Diamond.

Ambapo Wema Sepetu aliamua kujibu tuhuma hiyo aliyotupiwa na Mange na kumwambia aache kuji[pendekeza kwake na anatakiwa amshauri vyema Hamisa juu ya mambo haya anayoyapitia.

Wema na Mange wameingia katik amalumbano makali mara baada ya Wema Sepetu kuonesha kufurahia kwa kile kilichomkuta Hamissa na Mange Kimambi akijaribu kumkingia kifua Hamisa Mobettpo ambaye anashambuliwa mtandaoni kufuatia kuvuja kwa sauti hizo.

 

 

 

UEFA yaombwa kubadili sheria za bao la ugenini, usajili
Katibu Mkuu CCM amnyoshea kidole Makonda