Kiungo kutoka nchini Burkina Faso Ismail Sawadogo amewajibu baadhi ya Mashabiki wanaobeza kiwango chake, hasa baada ya kushindwa kutumika ipasavyo katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu FC, uliopigwa Jumatatu (April 10).

Sawadogo alishindwa kuendelea na mchezo huo uliopigwa Highland Estate, baada ya Kocha Robertinho kumtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Kiungo kutoka Tanzania Nassoro Kapama.

Kiungo huyo aliyesajiliwa Simba SC wakati wa Dirisha Dogo la Usajili amesema baadhi ya Mashabiki wameshindwa kuelewa kilichotokea katika mchezo huo, ambao Mnyama alichomoza na ushindi wa 2-0 dhidi ya Ihefu FC.

Amesema hakutoka mchezoni, lakini kilichotokea ni jambo la kawaida kwa mchezaji yoyote duniani, hivyo halimpi shida nab ado anaamini ana nafasi nyingine ya kuitumikia Simba SC katika michezo ijayo.

“Siwezi kutoka mchezoni naelewa kutolewa kikosini ni kawaida. Mimi sio wa kwanza kutolewa mapema, naelewa hilo na haliniondoi kuwa nina uwezo wa kucheza. Nahitaji muda zaidi ili kuweza kuonyesha uwezo wangu,”

“Niliondolewa labda sikufiti kile kocha alikuwa anatamani kuona nikikifanya. Lakini najiamini na natamani kupewa nafasi ya kucheza ili niweze kuonyesha uwezo wangu, kitendo cha kukaa benchi kwa muda mrefu pia ni tatizo.” amesema Sawadogo

Mabao ya Simba SC katika mchezo huo yalikwamishwa wavuni na Mshambuliaji kutoka DR Congo Jean Baleke katika kipindi cha pili na kuiwezesha klabu hiyo kuendelea kukaa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ikifikisha alama 60, ikitanguliwa na Young Africans yenye alama 68.

Tanzania mwenyeji wa ngumi Afrika
Mapigano ya kikabila yauwa 24, nyumba zachomwa moto