Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi, Clearence Seedorf ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Deportive La Curuna inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Hispania mpaka mwisho wa msimu.
Kiungo huyo aliyewahi kuichezea Ajax, Real Madrid na AC Milan, amechukua nafasi ya Cristobal Parralo ambaye amefukuzwa siku ya jumapili baada ya kufungwa na Real Sociadad mabao 5-1 na kuiacha timu hiyo katika nafasi za mwisho.
Seedorf mwenye umri wa miaka 41 ameshafundisha timu mbili mpaka sasa ikiwemo AC Milan aliyo isimamia kwa michezo 22 kuanzia mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa sita 2014. TImu nyingine aliyo ifundisha ni Shenzhen inayoshiriki ligi daraja la pili nchini China.
Seedorf alipata mafanikio wakati akiwa mchezaji kwa kufanikiwa kuchukuwa klabu bingwa barani ulaya akiwa na timu tatu tofauti,na pia mataji ya ubingwa wa ligi za nchi tatu tofauti.