Komputa zenye dhamani ya sh. Milioni 3.2 aina ya HP zimetolewa kwa shule ya Sekondari ya Ukwamani Jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kuwafanya wanafunzi kusoma kwa maharifa na weredi zaidi.

Vifaa hivyo vya utendaji kazi kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Ukwamani vilitolewa Dar es Salaam na mdau wa Elimu Devid Kayuni.

Hata hivyo mdau huyo wa elimu aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa malengo na kusema kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha kwani wakiendeleza Michezo bila kusoma wadau hao watashindwa kuwasaidia.

Aidha Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ukwamani Safina Egha, pamoja na mambo mengine alicia pongezi zake za dhati na kuwataka wadau wengine kujitokeza kwa wingi.

Watu watano wafariki kwa ajali Tanga
Haya hapa matokeo ya Darasa la 7 2020