Muungano wa sekta ya filamu za ngono nchini Japan umeomba msamaha na kuahidi kuifanyia mabadiliko sekta hiyo kufuatia madai kwamba wanawake wanalazimishwa kufanya ngono katika filamu.

Muungano wa kunadi picha hizo umesema kuwa unaomba msamaha kwa kushindwa kujichukulia hatua .

Hatua hiyo inajiri baada kundi la wanaharakati kuwaonya wanawake ambao wanateswa katika sekta hiyo.

Sekta hiyo ya filamu za ngono nchini Japan imekuwa ikikashifiwa kwa unyanyasaji wa haki za kibinaadamu.

Lakini shaka kuhusu mfumo wa sheria unawafanya waathiriwa kushindwa kujitoa na kulalamikia tatizo hilo.

Mnamo mwezi Machi,shirika moja la haki za kibinaadamu,lenye makao yake mjini Tokyo lilisema kuwa linajua kuhusu ongezeko la visa ambavyo wanawake walio na matumaini ya kuwa wanamitindo wanalazimishwa kujihusisha katika kanda za video zilizo chafu

Wanajeshi Wa Sudan Kusini Waiba Chakula
Wapishi Wa pizza Watakiwa Kwenda Shule Kusomea Upishi