Mwanariadha machachari na anayefanya vizuri katika mchezo huo, Caster Semenya na wa baadhi ya wanariadha wengine wenye homoni nyingi za kiume inatarajiwa kujulikana hivi karibuni mara baada ya ripoti ya utafiti kutolewa.
Ripoti hiyo ya utafiti iliyotolewa imesema kuwa wanawake wanaozaliwa na homoni nyingi za kiume (Testosterone}wanauwezo mkubwa wa utendaji kazi ikilinganishwa na wenzao katika mashindano hayo ya mbio.
Aidha, ripoti hiyo iliyochapishwa na jarida la matibabu katika michezo inatokana na Sampuli 100 za damu zilizochukuliwa kutoka kwa wanariadha mbalimbali kwa muda wa miaka miwili.
Hata hivyo, ripoti hiyo imekuja siku chache mara baada ya mahakama ya usuluhishi wa mchezo wa riadha IAAF kuwapiga marufuku wanariadha wa kike walio na homoni nyingi za kiume yaani testosterone.