Kocha kutoka nchini Ureno Carlos Queiroz ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Kocha Mkuu wa Timu ya taifa ya Misri, saa chache baada ya kikosi cha nchi hiyo kushindwa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia, zitakzounguruma baadae mwaka huu nchini Qatar.

Misri ilipoteza nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo mwaka 2018 kule nchini Urusi, kufuatia kupoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Senegal uliounguruma jana Jumanne (Machi 29) mjini Dakar- Senegal.

Kocha Queiroz amesema ni wakati wake kuwajibika kama mkuu wa Benchi la ufundi la Misri, baada ya kushindwa kutimiza wajibu wa kuivusha nchi hiyo hadi kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2022.

Amesema Chama cha Soka nchini Misri kilimuwezesha kwa kila hatua ili kufanikisha timu ya taifa ya nchi hiyo inafuzu, lakini kushindwa kwake, ni dhahir anaamini hana maana tena katika soka la nchi hiyo.

Carlos (69) alijiunga Kuitumikia September 08, 2021 na Sasa Ameamua Kujiwajibisha yeye Mwenyewe kwa kushindwa kufuzu kucheza kombe la Dunia 2022 huko Qatar.

Misri waliondoshwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-1, na kuiacha Senegal ikiungana na mataifa mengine manne kutoka Afrika ambayo yatashiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar.

Mataifa mengine ya Afrika yaliyofuzu ni Morocco, Ghana, Cameroon na Tunisia.

Dkt. Mabula ataka elimu itolewe ugawaji wa ardhi
Waziri Dkt. Ndumbaro azungumza na Balozi wa Marekani Dkt. Wright kuhusu uwekezaji maeneo ya wanayapori