Wizara ya ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza kufanya mabadiliko ya kalenda ya mihula ya wanafunzi wa awali,msingi na sekondari ambapo wanafunzi hao wote watapumzika kuanzia Julai 29 hadi Septemba 4, kupisha Sensa ya Watu na Makazi itakayofanywa Agosti mwaka huu.
Kauli hiyo ni kwa mujibu wa Waraka wa Elimu namba 1,wa mwaka 2022 unaohusu Kalenda ya Muhula kwa Shule za Awali, Msingi na Sekondari mwaka 2022 uliotolewa jana na Kamishna wa Elimu, Dk Lyabwene Mtahabwa .
Katika Waraka huo, wanafunzi wote watapumzika kuanzia Julai 29,mwaka huu hadi Septemba 4,mwaka huu ili kupisha zoezi la Kitaifa la Sensa ya Watu na Makazi iliyopangwa kufanywa Agosti mwaka huu.