Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye amekizungumzia kitendo cha baadhi ya wabunge wa upinzani bungeni kutoka tukoka nje ya bunge wakidai kukosa imani na Naibu spika Dk. Tulia Ackson.

Hizi hapa Sentensi tatu za Waziri Nape Nnauye

Wingereza wanasema mtu mwenye akili ndogo anajadili watu, wenzetu wana mgogoro na naibu spika lakini zipo njia za kibunge za kutatua huu mgogoro lakini wao hawataki kuzifuata, hii ni ishara kuwa wanaongozwa na akili ndogo” – Waziri Nape Nnauye

Lakini la pili kubwa linalosikitisha ni kuwa anayewaongoza kutoka na kuingia Freeman Mbowe haji, havai makaratasi kama wenzake na huwenda yupotu nyumbani amelala nyumbani kwake. Ushauri wangu wajaribu kuwa na akili kubwa kidogo ya kushughulika na mfumo” –Waziri Nape Nnauye

Baya kuliko yote ni kwamba wanawanyima fursa watu waliowachagua, utaona wameuliza maswali ambayo ilitakiwa yajibiwe na wao wakiwepo na hii ni salamu kwamba katika uchaguzi ujao tuweke watu ambao watajua wametumwa na wananchi” –Waziri Nape Nnauye

Watatu Wakatwa Uchaguzi Mkuu Stand Utd
Lowassa ampongeza Rais Magufuli kwa hili