Wakati akilaumiwa kufanya maamuzi ya kwenda kukutana na kocha wa Al Ahly, Senzo Mazingiza Mbata amerudisha majibu kwa waliomsemea mbovu kwa kitendo alichokfanya siku moja kabla ya Simba SC haijakutana na Al Ahly kwenye mchezo wa mzunguuko wa pili wa Kundi A wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika jijini Dar es salaam.
Senzo amejibu lawama alizotupiwa alipohojiwa na kituo cha Radio cha EFM kwa kusema: “Hakukuwa na siku nyingine ambayo ningeweza kuonana naye zaidi ya Jumatatu, (nisingeweza kuonana naye wikiendi na nisingeweza kuonana naye Jumanne kwa sababu walikuwa na ratiba ya kusafiri) Ni kitu gani ambacho naweza kumuambia Pitso Mosimane ambacho yeye hajui?”
“Kwa kifupi nilikutana na rafiki yangu ambaye sijaonana naye muda mrefu..nilionana naye sehemu ya wazi ambayo kila mtu anaona na nilikunywa naye kikombe cha kahawa….lakini naelewa niko kwenye ulimwengu wa Tanzania….” alisema Senzo na kuongeza kuwa kuonana naa kocha wa Al Ahly haikuhusiana na kabisa na mechi ya Simba SC ambao walishinda bao moja kwa sifuri.
Mwishoni Senzo akaongelea mchezo huo kwa kusema ilikuwa mchezo mkubwa na nzuri sana. Amesema watu waache mambo ya ‘Usimba’ na ‘Uyanga’ wajifunze kwa malengo ya kuendeleza mpira wetu.