Mshauri mkuu wa Uongozi wa Young Africans Senzo Mazingiza Mbata ameandika ujumbe wenye utata kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, ambao unadhaniwa huenda likawa dongo kwa wanaoendelea kupanga mipango ya kumkwamisha katika kazi zake ndani ya klabu hiyo.

Senzo ambaye aliachana na Simba SC mwezi Septemba 2020, ameandika ujumbe huo akitumia neno ‘VUVUZELA’, huku akiwahusisha wadau wa soka la Bongo ambao wanaopambana kuharibu mipango ya mabadiliko ya Young Africans.

Ujumbe huo wa Senzo unasomeka: “Vuvuzela hutumiwa kwa kawaida kwenye mechi za mpira wa miguu huko Afrika Kusini, na imekuwa ishara ya mpira wa miguu wa Afrika Kusini….

”Vuvuzela hii hutoa kelele nyingi kwa kuchangiwa na kelele za mashabiki … nimejifunza tu kwamba kuna tabia ya kibinadamu ya pembe hii hapa Tanzania ambayo inafanya kelele nyingi katika juhudi za kuharibu mipango ya @yangasc kwa MASHABIKI wake. Kweli, tuko kwenye njia sahihi na iliyojazwa ukweli na tunajua tunakoelekea.”

Hata hivyo mpaka sasa inahisiwa huenda amewalenga baadhi ya watu ambao wanapambana kumkwamisha kwenye mikakati yake ya kusaidia mabadiliko ndani ya Young Africans.

Lakini wadau wa soka nchini wanaendelea kufanya subra kwa kuamini ipo siku ukweli utadhihiri na itafahamika Senzo alikua anamaanisha nini kupitia ujumbe huo aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Diamond aingilia kati Simba Super Cup
Stendi ya Mbezi Louis kuanza kutumika