Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Senzo Mazingisa Batha, amewashusha Presha Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kufuatia tetesi zilizozuka mapema leo Alhamis (Juni 30), kuhusus kuuzwa kwa Mshambuliaji Fiston Kalala Mayele.
Mayele ametajwa kuwa kwenye Rada za klabu ya Kaizer Chief, huku tetesi zikieleza tayari Klabu hiyo imejipanga kumng’oa Jangwani kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Afrika Kusini.
Senzo amesema taarifa za Mshambuliaji huyo kuwa kwenye mpango wa kusajiliwa na Kaizer Chief hazina ukweli, na kama itatokea atauzwa klabuni hapo, basi yeye kama Mtendaji Mkuu ataondoka na kwenda kufanya kazi nyingine.
“Sijui hizi taarifa zinatokea wapi. Fiston Mayele haendi kokote ni mchezaji wa Young Africans na msimu ujao tutaendelea kuwa naye.”
“Kuna wachambuzi wawili kutoka Ghana ndiyo wanaotuvuruga sana, kwa kubuni hizi taarifa na kuzirushwa kwenye mitandao ya kijamii.” Amesema Senzo
Fiston Mayele ampongeza George Mpole
Mayele pia aliwahi kuhusishwa na taarifa za kuwania na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika RS Berkane mwezi uliopita, taarifa ambazo Uongozi wa Young Africans ulizikanusha kupitia vyombo vya habari vya Tanzania.