Mshauri wa uongozi wa Young Africans, Senzo Mazingiza Mbatha ametuma salamu kwa waajiri wake wa zamani Simba SC kuelekea mchezo wa fainali Kombe la Shirikisho ASFC utakaochezwa Julai 25, mkoani Kigoma.

Simba SC watatetea taji la ASFC kwa kuivaa Young Africans kwenye mchezo huo, ambao utapigwa katika dimba na Lake Tanganyika, Kigoma.

Senzo amesema Young Africans inafahamu kuwa, Simba SC imepania kulipa kisasi, baada ya kufungwa mchezo wa Julai 03, bao 1-0, hivyo wamejipanga na hilo.

“Tunajua wamepania kulipa kisasi, hizo ni hesabu zao na sisi Yanga tuna zetu, kuna wakati unaweza kupania kupata kitu na kisha usikipate na hatupo tayari kuliruhusu hilo.”

“Tunahesabu kubwa sana katika mchezo huu wa fainali tunataka kuufunga msimu kwa mafanikio zaidi, tunahitaji kuongeza kombe lingine ili tuwe na kitu fulani cha tofauti zaidi kufanikia hayo ni lazima tushinde tena,”

“Naijua Yanga sasa, ukiangalia huku juu kwenye uongozi kuna umoja mkubwa sana, viongozi wote sasa wanazungumza kitu kimoja lakini wanachama na mashabiki wetu nao hawako mbali na timu yao wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanaipigania timu yao.”

“Hii ni hali fulani ambayo inavutia sana hapa ndio unapokamilisha kuiita timu ya wananchi kwa kuwa wananchi na viongozi wao wako kwa ajili ya timu yao.”

“Kwenye timu nako maandalizi yanaendelea tunafuatilia kila hatua maendeleo ya timu yetu na wachezaji wanajua umuhimu wa kushinda mechi kama hii kubwa kuna utamu wa aina gani wanaupata na wanajua wanapata kutokana na nguvu ya wadhamini wetu hasa GSM ambao wanafanya kila kitu kuhakikisha akili ya wachezaji inakuwa katika kupigania ushindi.” amesema Senzo Mbatha Mazingiza

Senzo aliwahi kuwa Afisa Mtendaji Mkuu Simba SC, kabla ya kutimkia Young Africans mwanzoni mwa msimu huu, na nafasi yake ikajazwa na Barbara Gonzalez.

Manara ataja kikosi bora VPL 2020-21
Dili la Haaland laota mbawa