Ni siku ya pili ya mwanzo wa Wiki ya Kimataifa ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama kwa mtoto, kaulimbiu ni “Tufanye unyonyeshaji kazini, ufanye kazi,” Mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto – UNICEF, na la Afya Ulimwenginu – WHO, yanasisitiza haja ya usaidizi mkubwa wa unyonyeshaji katika sehemu zote za kazi.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na wakuu wa mashirika hayo, Catherine Russell wa UNICEF na Dkt. Tedros Ghebreyesus wa WHO huko Geneva, Uswisi na New York, Marekani inasema hatua hiyo ni muhimu, ili kuendeleza na kuboresha maendeleo katika viwango vya unyonyeshaji duniani kote.

Wanasema, “katika miaka 10, nchi nyingi zimefikia maendeleo makubwa ya kuongeza viwango vya akina mama kunyonyesha Watoto wao. Ingawa hivyo maendeleo makubwa zaidi yanawezekana pindi hatua za akinamama kunyonyesha Watoto zinalindwa na kupata usaidizi hasa pahala pa kazi.”

Aidha, ongezeko hilo limekuwa kwa takribani asilimia 10 na kufikia asilimia 48 ambapo nchi kama Cote d’Ivoire, visiwa vya Marshall, Ufilipino, Somalia na Vietnam zimepata ongezeko kubwa na kudhihirisha kuwa maendeleo yanaweza kuwepo iwapo unyonyeshaji wa mama kwa utalindwa na kupewa usaidizi.

Al-Hilal kutibua dili la Sofyan Amrabat
John Noble aipa jeuri Tabora United