Baada ya mlango wa kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu ujao kupitia CHADEMA, tayari wagombea wanne wamejitokeza miongoni mwao ni Lazaro Nyarandu na Mbungea wa Iringa mjini Peter Msigwa.
Nyalandu na Msigwa jana, kwa nyakati tofauti walipata nafasi ya kutaja vipaombelele vyao ambapo Msigwa ametaja vitatu na Nyalandu ametaja 25.
Msigwa amesema ana nia ya kuikwamua nchi, hoja yake si kwamba hakuna kitu hata kimoja kilichofanywa na utawala wa CCM, bali ukweli ni kwamba chini ya Serikali zote za CCM, nchi imeendelea kusuasua kimaendeleo kwa muda mrefu
Anasubiri chama chake kiweze kumpa ridhaa ya kugombea, na kama atapata nafasi hiyo amesema anakuja na vipaumbele vitatu, kufanya Mageuzi Makubwa ya Kielimu, kujenga Utawala Bora na Uwajibikaji na tatu ni kufanya Mageuzi Makubwa ya Uchumi wa Kisasa
Kada na Mwenyekiti wa chama hicho kanda ya kati, Nyalandu amesema ana vipaombele 25 ambavyo atavitekeleza ndani ya siku 10 pekee endapo watanzania watamchagua kuwa Rais 2020.
“Nasimama mbele yenu na mbele ya umma wa Watanzania, huku moyo wangu ukiwa umejaa shahuku kubwa nikitamani kuiona Tanzania, nchi tuipendayo kwa moyo wote inapata ustawi na kuendeleza matamanio, matarajio na ndoto za watu wake”. Amesema Nyalandu
Ameeleza wakati Tanganyika inapata Uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa kiingereza Mwaka 1961, Baba wa Taifa alisema “Tuwashe mwenge na tukauweke Kilimanjaro ili uangaze ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu, palipo na chuki kukawe na furaha, palipo na giza kukawe na Nuru” ambapo hiyo ndiyo asili ya watanzania na inapaswa kiwa hivyo daima
Ameongeza ” Watanzania wana matamanio na ndoto za maendeleo, vijana wao wana vipaji lukuki na wamejawa na uthubutu katika kutafuta maisha na kujiendeleza, huku wakiamini katika ahadi ya ukuu wa Taifa lao”.
Nyalandu aliwahi kuwa Waziri wa maliasili na utalii enzi za utawala wa awamu ya nne wa Rais Jakaya Kikwete, alikuwa Mbunge wa Singida kaskazini kupitia CCM tangu mwaka 2000 Hadi octoba 30 2017 alipo tangaza kujiunga na CHADEMA.