Mwanadada kutoka nchini Marakani, Serena Jameka Williams ameingia katika hatua ya fainali baada ya kumchakaza mpinzani wake Maria Sharapova, ambaye alidhaniwa huenda angempa tabu katika mchezo wa hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya Wimbledon Championship inayoendelea jijini Londo, Uingereza.

Serena alimbamiza Sharapova kwa urahisi kwa kumshinda kwa seti mbili kwa sifuri ambazo ni 6-2 na 6-4.

Ushindi huo unamuwezesha Serena mwenye umri wa miaka 33 kucheza mchezo wa fainali wa michuano ya Wimbledon kwa mara ya nane, hatua ambayo ni kubwa katika historia yake.

Mchezo wa fainali kwa wanawake umepangwa kufanyika kesho, ambapo Serena atapambana na mwanadada kutoka nchini Hispania, Garbine Muguruza ambaye alimshinda mpinzani wake kutoka nchini Poland, Agnieszka Radwanska katika mchezo wa hatua ya nusu fainali.

Kwa upande wa wanaume, leo hatua ya nusu fainali itachezwa ambapo bingwa mtetezi wa michuano hiyo Novak Djokovic, atapambana na Richard Gasquet huku mwenyeji Andy Murray akionyeshana ubabe na Roger Federer kutoka nchini Uswiz.

Gerrard: Sterling Shika Adabu Yako, Liverpool Ina Wenyewe
Recho Ajibu Tuhuma Za Kutumia Dawa Za Kulevya