Mcheza Tennis nguli duniani, mwanadada Serena Williams amethibitisha kuwa na ujauzito kupitia Met Gala.

Bingwa huyo mara 23 wa Grand Slam aliwaambia waandishi wa habari kwenye onyesho la mitindo la New York kwamba kuna ‘watatu kati yetu’ kwenye zuria jekundu wakati akiwasili na mume wake, Alexis Ohanian. Wawili hao walipata mtoto wao wa kwanza, Olympia, Oktoba mwaka 2017.

Williams aliandika katika jarida la Vogue mwaka jana kwamba anataka kuachana na tenisi na kuweka mkazo wa kuendeleza familia yake.

Met Gala ni mwaliko wa mwaka wa mitindo wenye lengo la kukusanya fedha, uliofanyika kwenye jumba la kutunza kumbukumbu za kazi za sanaa.

Katika mtandao wa Tik Tok, Williams alisema kuwa ana furaha wakati Anna Wintour alipowaalika watu kati yao katika Met Gala.

Mhariri Mkuu wa jarida la Vogue, Anna Wintour alikuwa mwenyekiti wa tamasha hilo lililofanyika jioni na ni rafiki wa karibu wa Williams, ambaye mara kwa mara anahudhuria tukio hilo.

Bingwa wa tenisi, Roger Federer pia alihudhuria tukio hilo. Sambamba na mwenyekiti mwenza wa tukio hilo, Wintour na mshindi wa tuzo za Grammy Dua Lipa, mwanamitindo Penelope Cruz na mwandishi, mwigizaji na mzalishaji Michaela Coel walikuwepo.

Mlimbwende Karlie Kloss pia alithibitisha ujauzito wake wa pili kwenye tukio hilo.

GGML kampuni kinara uzingatiaji wa malengo SDGs
Kocha Marumo Gallants kuitumia Simba SC Dar