Serena Williams ameendelea kudhihirisha ubora wake kwa kuibuka mshindi kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya US Open inayoendelea nchini Marekani.

Serena alikua na kibarua cha kumkabili dada yake wa damu Venus Williams, na amefanikiwa kumshinda kwa kumbamizwa kwa seti mbili kwa moja ambazo ni 6-2, 1-6 na 6-3.

Kabla ya mchezo huo wawili hao walitambiana huku Venus akionyesha kuwa na kusudio la kumshinda mdogo wake, lakini mambo yalimgeukia na kuonyesha bado ana safari ndefu ya kutimiza lengo la kumsimamisha Serena.

Hata hivyo haikua kazi rahisi kwa Serena kuhitimisha ushindi kwa njia rahisi, kwani ilimlazimu kusubiri hadi katika seti ya mwisho, baada ya ndugu yake kusawazisha katika seti ya pili na kuwa seti moja kwa moja.

Ushindi huo unemuwezesha Serena kusonga mbele na atapambana na mwanadada kutoka nchini Italia Roberta Vinci, ambaye alimshinda mpinzani wake kutoka nchini Ufaransa Kristina Mladenovic kwa seti mbili kwa moja ambazo ni 6-3, 5-7 na 6-4.

Matokeo ya michezo mingine ya hatua ya robo fainali upande wa washiriki wa kiume.

Marin Čilić  kutoka nchini Croatia alimshinda Jo-Wilfried Tsonga kutoka nchini Ufaransa kwa seti tatu moja ambazo ni 6–4, 6–4, 3–6, 6–7 na 6–4.

Novak Djokovic kutoka nchini Serbia amemshinda Feliciano López kutoka nchini Hispania kwa seti tatu kwa moja ambazo ni 6–1, 3–6, 6–3 na 7-6

Michezo mingine ya hatua ya robo fainali itachezwa hii leo upande wa wanawake itashuhudiwa;

Petra Kvitová kutoka Jamuhuri ya Czech watapambana na Flavia Pennetta kutoka nchini Italia.

Victoria Azarenka kutoka nchini Belarus atapambana na Simona Halep kutoka nchini Romania.

Upande wa wanaume;

Stan Wawrinka kutoka nchini Uswiz atavaana na Kevin Anderson kutoka Afrika kusini.

Richard Gasquet kutoka nchini Ufaransa atapambana na Roger Federer kutoka nchini Uswiz.

Bomu La Gwajima Limempata Dk. Slaa?
Rooney Ampiku Sir Bobby Charlton England