Mwanadada Serena Williams, anatarajiwa kuamliza mwaka 2015 akiwa katika nafasi ya kwanza kwa ubora duniani upande wa wanawake, baada ya viwango vya ubora kutolewa usiku wa kuamki hii leo.

Serena bado yupo kileleni kwa sasa na anatarajiwa kuwa na mwisho mzuri kwa mwaka huu, endapo atafanya vyema kwenye michuano ya wazi ya Marekani *Us Open* ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi lake mwanzoni mwa juma lijalo.

Serena kama atafanikiwa kufanya vyema na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya nne mfululizo baada ya kufanya hivyo mwaka 2012, 2013, 2014 ataendelea kuitetea nafasi yake ya kwanza kama ilivyo matarajio ya walio wengi ulimwenguni kote.

Endapo itakua kinyume na hapo huenda Serena akaporomoka na kumaliza mwaka katika nafasi za chini.

Hali kama hiyo ipo kwa Novak Djokovic ambaye bado anaongoza katika orodha ya ubora wa viwango upande wa wanaume, na kama mambo yatakuwa mazuri mwenye michuano ya US Open atatetea nafasi yake ya kwanza.

Orodha ubora wa viwango iliyotolewa usiku wa kuamkia jana kwa upande wa wanaume inaonyesha.

1 Novak Djokovic (Serbia), 2 Roger Federer (Uswiz), 3 Andy Murray (Scotland), 4 Kei Nishikori (Japan), 5 Stan Wawrinka (Uswiz), 6 Tomas Berdych (Jamuhuri ya Czech), 7 David Ferrer (Spain), 8 Rafael Nadal (Spain), 9 Marin Cilic (Croatia), 10 Milos Raonic (Canada)

Kwa wanawake viwango vya ubora duniani vinaonyesha.

1 Serena Williams (USA), 2 Simona Halep (Romania), 3 Maria Sharapova (Russia), 4 Caroline Wozniacki (Denmark), 5 Petra Kvitova (Jamuhri ya Czech), 6 Lucie Safarova (Jamuhuri ya Czech), 7 Ana Ivanovic (Serbia), 8 Karolina Pliskova (Jamuhuri ya Czech), 9 Garbine Muguruza (Spain), 10 Carla Suarez Navarro (Spain)

Msenegal Mpya Wa Simba Ashuka Dar es salaam
Jordin Spark Aifunza Billboard Kuandika Habari, Ni Baada Ya Kumtibua