Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora katika Bara la Afrika kwa mwaka 2020.


Tuzo hizo zimetangazwa siku ya Jumatatu na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani kwa njia ya Mtandao.

Serengeti: Mwanafunzi afariki kwa kukanyagwa na Tembo

Hii ni mara ya pili kwa Hifadhi ya Taifa Serengeti kushinda katika kundi la hifadhi zinazoongoza kwa ubora zaidi barani Afrika baada ya kunyakua tuzo hiyo mwaka 2019.

Serengeti imeibuka mshindi katika shindano lililoshindanisha hifadhi nyingine za Central Kalahari (Botswana); Etosha (Namibia); Kidepo Valley (Uganda) Kruger (Afrika Kusini) na Maasai Mara (Kenya).

Serengeti ni maarufu kwa msafara wa nyumbu wahamao zaidi ya milioni moja na nusu, aina mbalimbali za wanyamapori wanaopatikana kwa wingi, mandhari nzuri ya kuvutia pamoja na shughuli mbalimbali zinazowavutia watalii wengi.

Marekani: Mwanasheria Mkuu aunga mkono hoja ya Trump
Rais wa zamani wa Mali afariki