Klabu ya Borussia Dortmund (Ujerumani) na Newcastle United (England) zimeingia kwenye mchakato wa kuiwania huduma ya Mshambuliaji wa Stuttgart, Serhou Guirassy ambaye hadi sasa amefunga mabao 16 tangu kuanza kwa Ligi Kuu nchini Ujerumani msimu huu 2023/24.

Staa huyu wa kimataifa wa Guinea mwenye umri wa miaka 27, awali alitajwa kuwa kwenye rada za Brentford ambayo inamtaka akawe mbadala wa lvan Toney, vilevile Manchester City, Man United na Newcastle United.

Inaelezwa kuwa Serhou ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, ana kipengele ambacho kinamruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa chini ya Euro 30 milioni.

Hadi sasa mchezaji huyu hajaweka wazi ikiwa anaondoka au atabaki hadi mwisho wa msimu ingawa timu nyingi zimeonyesha mpango wa kutaka kumchukua.

Mbali ya mabao l6 aliyofunga kwenye Bundesliga, pia amefunga mabao mawili kwenye mechi za DFB-Pokal.

Ukatili: Polisi yaelimisha uchangiaji damu
Mfumo haulengi kumuondoa mtu kazini - Kikwete