Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema kuwa Serikali ya Tanzania haitavumilia taasisi yeyote ambayo itaonyesha nia ya kukwamisha zoezi la kuwarejesha wakimbizi, wanaotokea nchi jirani ya Burundi.
 
Lugola ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Kigoma alipotembelea kambi ya Wakimbizi Nduta, iliyopo wilayani Kibondo mkoani humo akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Burundi.
 
“Wakimbizi wa Burundi wanaoishi Tanzania, wanalelewa vizuri sana na mpango wa Serikali ni kuwarejesha nyumbani kwao Burundi, kwa kuwa sasa kuna amani.”amesema Lugola
 
Aidha, Waziri Lugola amesema Serikali katika kila wiki itakuwa ikiwarudisha wakimbizi 2000 mpaka pale watakapoisha.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 26, 2019
Maalim Seif akamatwa na Polisi