Serikali: Bado hatujaondoka kwenye mpango wa kusamehewa madeni

Dkt Kijaji ameyasema hayo Jumatano hii bungeni kufuatia swali lilioulizwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe lililohoji: Je, serikali inafikiria nini kuhusu deni la taifa wakati kipindi cha awamu ya tatu cha mheshimiwa Mkapa ambapo deni la taifa liliweza kusamehewa mpaka kuwa chini ya dola bilioni kumi? na Je, ni kwanini serikali sasa hivi isione uwezekano na isifanye initiative ya madeni na kurudi katika shughuli kimaendeleo?

Akijibu swali hilo, naibu waziri alisema: Serikali haijaondoka katika mpango huo wa kusamehewa madeni na bado tunaendelea na mchakato huu kwa kushirikiana na IMF pamoja na World Bank. Zipo nchi zilizokuwa na mpango wa kuhakikisha tunasamehewa katika nchi yetu lakini zilisitisha kutokana na migogoro katika nchi hizo ikiwa ni nchi ya Iraq, Iran pamoja na nchi nyingine zenye migogoro ambazo zilisitisha sasa kusamehewa madeni, hivyo bado tunaendelea na mchakato wa kuwashawishi wadau hao wa maendeleo ili waweze kutusamehe madeni haya.”

Wakati huo huo waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, aliweza kumpongeza naibu waziri wa fedha kwa kutoa ufafanuzi huo wa kina huku akiwatoa hofu wananchi kwa neno ambalo alilitoa mheshimiwa Mbowe kuhusu kuligawa deni hili kwa kila Mtanzania.

Mheshimiwa Nchemba alisema: Ukiligawa deni hilo kwa kila mtanzania, kwanza hakuna siku ambapo watanzania watagongewa mlango wakigawanywa deni hilo la taifa, na wala katika taifa lolote hakuna utaratibu wa kupima deni kwa kuangalia ujazo wa watu, bali deni la taifa linapimwa kufuatana na uwezo wa nchi kimapato na jinsi inavyoweza kuservice deni hilo.”

“Kwa maana hiyo tunapoangalia kukuwa kwa deni tunatakiwa kuangalia miundo mbinu ya nchi yetu imekuwa kwa kiwango gani,kwasababu wazo hilo linatokana na miundo mbinu ya nchi,” aliongeza.

Video: Serikali kuvifungia Vyuo vinavyotoza ada kwa fedha za kigeni
Nicklas Bendtner Arejea England