Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kuvunja Jiji la Dar es Salaam na kuchagua manispaa moja katika jiji hilo itakayopandishwa hadi na kuwa Jiji huku lengo likiwa kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Ameyasema hayo wakati akizindua barabara za juu ‘Kijazi Interchange’ zilizopo ubungo Jijini Dares Salaam leo Jumatano Februari 24, 2021.

“Ninategemea kuvunja Jiji la Dar es Salaam ili tutengeneze jiji la eneo fulani tunaweza kuifanya Ilala ndio iwe jiji itategemea na namna mambo yatakavyokwenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu wanachangiwa fedha na hawana miradi ya maendeleo hili nitalikataa.”amesema Rais Magufuli

“Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa. Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani na ninafikiri Ilala inafaa kuwa jiji maana ndio ipo katikati, Ubungo itasubiri maana barabara bado hazijatengenezwa,” amesema Rais Magufuli.

“Haiwezekani unakuwa na madiwani wamekaa tu wanatengewa bajeti hizo fedha ni vizuri zikapelekwa kwenye miradi ya maendeleo ya barabara hayo ni matumizi bora ya fedha za walipakodi kwa hiyo mjiandae kisaikolojia meya atapatikana katika manispaa ya Ilala,” amesisitiza.

Kiongozi, Wachezaji Namungo FC kuondoka Angola
Masau Bwire aipongeza Simba SC, 'MSIJISAHAU'