Serikali nchini imesema inafanya jitihada za kuboresha hali ya elimu likiwepo  suala la miundombinu elimu ya juu, kati, Sekondari na Msingi, na kuipitia mitaala iliyopo endapo inafaa kwa wakati wa sasa.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.  Leonard Akwilapo, jijini Dodoma, jana wakati akifungua mkutano wa mwaka wa tathmini ya Elimu

Amesema Wizara imekuwa ikifanya jitihada kuhakikisha kiwango cha elimu kinakua na kutoa elimu yenye ubora nchini, kwa kuanza maboresho ya miondombinu ya vyuo ya elimu ya juu, elimu ya Kati, Shule za Sekondari na Shule za Msingi.

“Tumekuwa tukiboresha hali ya elimu yetu, na kwa sasa tumeanza na maboresho ya miondombinu ili vitu hivi viende kwa pamoja, madarasa kwa vyuo vya Kati na shule zetu zote ikiwepo Mzumbe na UDSM” amesema Dkt. Akwilapo.

Kuhusu maboresho ya Mitaala, Dkt. Akwilapo amesema utaenda sambamba na ile ya shule za msingi na vyuo, kwa kuzingatia matwaka ya usasa, kwa wanafunzi kuweza kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.

Katibu Mkuu huyo amesema kwa sasa kiwango cha elimu nchini kimeimarika tofauti na awali na kwamba wengi wa wanafunzi wanaomaliza masomo ya sekondari hufanya vizuri katika mashindano ya taaluma nje ya nchi.

“Wapo watu bado wana dhana ya kwamba elimu yetu haina viwango, jambo hilo si kweli kwani wanafunzi wanaomaliza masomo yao hapa nchini wakienda nje hufanya vizuri na kuiletea sifa nzuri nchi yetu.” Ameongeza Dkt. Akwilapo.

Awali akiongea katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa mtandao wa Asasi za kiraia wadau wa elimu (TENMET), ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hakielimu John Kalage, amesema wanaridhishwa na hali ya elimu nchini.

“Na kupitia mkutano hu tutaangalia na kushiriki kujadili changamoto zilizopo katika elimu hasa ongezeko la udahili katika shule ili kusitokee athari za utoaji wa elimu isiyo bora kwa watoto wetu.” amefafanua Kalage.

Mkutano huo wa siku tatu, umewakutanisha wadau mbalimbali, asasi za kiraia, wafadhili na Wizara ya Elimu ambapo kwa pamoja wanatathmini malengo waliojiwekea.

Azam sasa kamili kuivaa Triangle Fc
Video: Antonio Nugaz amtumia salamu Haji Manara