Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amefika katika Kijiji cha Mpwayungu Wilayani Chamwino na kubaini changamoto mbalimbali za Wananchi ikiwemo maji, umeme, Barabara na kuzipatia ufumbuzi kero hizo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kusikiliza changamoto za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Senyamule ameyasema hayo katika Kijiji hicho na kuongeza kuwa ni matamanio yake kuona Rais Dkt. Samia yanatimia kwa kusikiliza changamoto walizonazo Wananchi na kuzipatia ufumbuzi ambazo zatawasilishwa kwa ajili ya utekelezaji.
Katika Hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akiwa katika mradi wa mashamba ya pamoja ya ‘Bulding a Better Tomorrow ‘(BBT) ametoa shime kwa wasimamizi wa mradi huo kuchukua hatua kwa Changamoto zinazojitokeza na kupelekea mradi huo kutokwenda kwa kasi iliyokusudiwa.
Kwa Upande Wake Mkuu wa Wilaya ya chamwino, Gift Msuya ameishukuru Serikali kwa kuendelea kufanya mambo ya maendeleo katika Tarafa ya Mpwayungu pamoja na mradi wa Kilimo cha pamoja, Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Nkhambako.