Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inazingatia Utawala Bora na Utawala wa Sheria kwani kwa kufanya hivyo ni kuendeleza msingi wa maendeleo ya uchumi.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima ameyasema hayo kwa niaba ya Rais katika Mkutano wa Sita wa Maombi ya Kitaifa chini ya Shirika la Kingdom Network Leadership uliozungumzia mkakati wa Maendeleo wa Kitaifa wa Miaka Mitano wa Utawala Bora na Sheria kama msingi wa maendeleo ya kiuchumi.

Amesema, kupitia kaulimbiu ya mwaka huu ya mkutano huo inayosema  “Nguvu ya Tabia katika Uongozi” anaamini kwamba Taifa haliwezi kujengwa bila uongozi wenye uadilifu, maadili na maadili hivyo watu wanapofanya kazi kwa uadilifu na kuwathamini wengine, kila mtu hupokea huduma zinazostahili kwa wakati na kuridhika.

“Tunahitaji uadilifu katika ukusanyaji wa kodi na mapato, usimamizi wa fedha za umma na uwajibikaji. Tunahitaji uadilifu katika uwekezaji na katika kushughulika na wawekezaji. Nimefurahia kuona kwamba KLNT imeweka pamoja mkutano huu wa Sala ya Kitaifa,” alisema Gwajima.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste – CCT, Askofu Stanly Hotay amewasihi viongozi kutafuta hekima zaidi na kujitoa kuwajali wengine na kuwa waadilifu.

“Unaweza ukawa na nafasi, nguvu na uwezo lakini ukaangushwa na tabia yako, tabia ndio msingi wa yote. Sifa namba moja ya mtu wa tabia njema ni upendo” amesema Askofu Hotay.

Naye Mratibu wa kongamano hilo, Isack Mpandwa amebainisha malengo ya Maombi hayo ya Taifa ambayo yanafanyika kwa mara ya sita mwaka huu kuwa ni kuliombea Taifa, kumshukuru Mungu na kuwaombea viongozi wa kitaifa.

Viongozi wengine waliohudhuria Mkutano huo ni Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Balozi Pindi Chana, Mbunge wa Jimbo la Nsimbo, Anna Lupembe, Mbunge viti Maalum, Ritha Kabati na Mbunge wa Serengeti, Amsabi Mrimi.

Wengine ni wageni kutoka nje ya nchi Prof. Patrice Lumumba wa Kenya, Mchungaji Dkt. Paul Enenche wa Nigeria na Mfanyabiashara maarufu Lloyd Ward.

Bilioni 24.4 zatengwa kuwasaidia waraibu dawa za kulevya
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 25, 2023