Spika wa bunge Job Ndugai, ameiagiza Serikali kujielekeza katika miradi mikubwa na miradi midogo na kuwaachia wawekezaji ama wananchi.

Spika Ndugai amesema hayo leo Mei 23, 2021 Bungeni Jijini Dodoma baada ya Naibu Waziri wa Mifugo kujibu swali la Mbunge wa Jimbo la Makete, Festo Sanga

Spika Ndugai, amesema ni jambo ambalo halipendezi machoni mwa watu kwa Serikali kuwa na miradi midogo zikiwemo ranchi zenye mifugo michache.

Aidha Spika amesema mradi mdogo kama huo kusimamiwa na Serikali ili hali una mifugo michache ambayo ingeweza kusimamiwa na wawekezaji ama wanakijiji.

Ametolea mfano wa ranch ya Kongwa amabyo amesema haina haja ya kuwa chini ya serikali kuu ilihali wananchi wananweza kuindeleza kiufanisi.

Rais Mwinyi afanya Uteuzi Zanzibar
Gomes: Simba inanidai