Serikali imetoa agizo kwa wakazi wote wanaoishi katika ardhi isiyorasimishwa na kusema kuwa kuanzia mwaka huu itatangaza kodi na kutaka wakazi wote kulipa kodi hiyo na kuhakikisha ardhi yao inapimwa.

Ambapo Serikali imetangaza kutoa kipindi cha muda maalumu, ndani ya huo muda inawataka wakazi wote wanaoishi katika ardhi isiyopimwa kuhakikisha makazi yao yanapimwa, kinyume na hapo Lukuvi ametangaza kuziagiza manispaa kufunga makazi yao.

Imesema wanaoishi katika makazi yasiyopimwa watatambuliwa kwa kupewa leseni za makazi zitakazo kuwa na ukomo, wakitakiwa kuishi kwa muda utakaopangwa.

‘’ Maeneo yote yasiyopimwa ambayo ni makazi holela watapewa leseni na baada ya muda Fulani yatatakiwa kuwa yamepimwa” amesema Lukuvi

Aidha imewataka wananchi kuunda kamati ya urasimishaji itakayosaidia kupima maeneo ya makazi yao.

‘’kamati hizo ni za wananchi wenyewe watakaoshughulika nazo, na fedha watakazokuwa wakizichanga zisiende halmashauri au wizarani kwani zitaibiwa’’ amesema Lukuvi.

Katika kuboresha utaratibu huo mpya na kudhibiti matapeli, serikali imesema itaanzisha mradi mpya katika manispaa ya kinondoni na Ubungo itayowezesha  kutoa hati miliki za ardhi hiyo kwa njia ya kielektroniki.

 

Bombadier yampagawisha Rais Museveni
Video: Shilole na ngoma yake mpya 'Kigori'