Serikali imeeleza kuwa inakusudia kuanzisha vituo vya kulea vipaji katika shule mbalimbali na katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, ili kuhakikisha vipaji vya watoto havipotei.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) inayofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Basghungwa amesema kuwa mashindano hayo ndiyo msingi wa kuvumbua vipaji na kwamba ili kufanya vizuri katika michezo mbalimbali, ni lazima uimara uanzie chini.

Aidha, amesema kuwa ili kukuza vipaji zaidi katika uzinduzi huu wamealikwa wavumbua vipaji kutoka vilabu mbalimbali nchini, Taasisi ya Mbwana Samatta na mawakala kutoka nchini Sweden.

Mashindano hayo yanaratibiwa na wizara tatu ambazo ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya TAMISEMI.

Polisi watangaza Mwezi wa kiama kwa wahalifu
Bomba lapasuka, maji kukosekana kwa saa 24