Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Serikali itaangalia namna ya kubadilisha Sheria ya Jumuiya ili kuwe na utaratibu wa utoaji wa huduma za Kiroho, hasa kutokana na kuwapo kwa utitiri wa Vibanda Imani.
Simbachawene amebainisha hayo alipozungumza kuhusu ajali iliyotokea Moshi, ambapo watu 20 wamepoteza maisha na wengine 16 wamejeruhiwa kwenye Kongamano la maombi la Bonifance Mwamposa.
Amesema pamoja na kongamano hilo kuwa na kibali cha siku tatu kilichoombwa na Mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa, lakini wanaonesha walikiuka masharti ya kibali ambacho ni kongamano kuendelea baada ya saa 12 jioni.
Na kusisitiza kuwa ili kuepukana na madhara makubwa zaidi siku zijazo, Wizara itaangalia namna ya kuifanyia marekebisho ya Sheria ya Jumuiya ambayo ndiyo inayotumika kusajili Taasisi za Dini.