Serikali imesema kuwa inatarajia kuja na utaratibu mpya wa kutibu ugonjwa wa Dengue ambao umezuka katika baadhi ya mikoa nchini ikiwemo Dar es Salaam na kupelekea vifo kwa baadhi ya watu na wengine kuugua.
Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mbunge wa Ilala Mussa Zungu ambaye alihoji juu ya Serikali kugawa dawa mpya zitakazomaliza mbu wa ugonjwa wa Dengue.
Akiuliza swali, Zungu amesema kuwa, bado kuna changamoto kwenye upambanaji wa ugonjwa Dengue, Serikali itabadilisha dawa zinazotumika ili wananchi washiriki wazimwage kwenye maeneo yao.
Akijibu swali hilo Bungeni, Waziri Ummy amesema kuwa, suala hilo limeshaanza kufanyiwa kazi na serikali.
“Suala hili limeanza kufanyiwa kazi na Serikali, ndani ya siku 2 tutatoa kauli rasmi jinsi gani tumechukua hatua za kupambana na Dengue,”amesema Ummy Mwalimu
-
Serikali kubuni njia mbadala ya kutibu ugonjwa wa Dengue
-
Tusiwanyanyase Wafanyabiashara hawa- IGP Sirro
-
Serikali yaokoa mabilioni uendeshaji mashauri ya madai
Waziri Ummy ameongeza kuwa hakuna njia nyingine ya kujikinga na ugonjwa Dengue zaidi ya kuwatokomeza mbu hao.