Leo Juni 11, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema tayari wapo kwenye mchakato wa kufanya marekebisho ya sheria za afya na uzazi ili kuwalinda wanawake na wanaume ambao wake zao wametoka kujifungua watoto kabla ya umri.
Amesema lengo likiwa ni kuwasaidia wazazi hawa ili waweze kupata haki ya kufanya malezi bora kwa watoto wao na malezi ya familia kwa ujumla.
“Naomba nilihakikishie Bunge lako tukufu kuwa, hayo ni mambo ambayo yanaendelea kujadiliwa na kufanyiwa kazi ili kuweza kuwasaidia wanawake lakini hata wanaume ambao wake zao wamejifugua watoto ambao wamezaliwa kabla ya umri wao, ili waweze kupewa haki na kusaidia malezi ya watoto na malezi ya familia kwa ujumla” amesema Waziri Mhagama.
-
TCRA yapiga ‘stop’ mitandao isiyojisajili kuhabarisha, Jamii Forum yatii amri
-
SSRA yatoa sharti zito kwa wanachama Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
Mhagma ameongezea kuwa Serikali itaendelea kubadili baadhi ya sheria za afya ya uzazi hasa kwa wamama wanaopata changamoto mbalimbali wakati wa kujifungua ili kuweza kuwasaidia wafanyakazi nchini.
Sheria ya Ajira na Mahusiano ya kazi ya mwaka 2004, inampa mama mjamzito ambaye ni muajiriwa likizo ya miezi mitatu kabla ya kujifungua, na atatakiwa kurudi kazini wiki sita baada ya kujifungua, pia sheria hiyo inatoa likizo ya siku tatu kwa baba wa mtoto baada ya mama kujifungua.