Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema, utaratibu wa kuzuia mikutano ya kisiasa isiyofuata Sheria na taratibu upo palepale.
Amesema, muda wa Siasa ukifika Serikali itaruhusu mikutano hiyo yenye lengo la kutoa nafasi kwa wanasiasa kuzungumza na wananchi na kueleza kwa wananchi walichokifanya kwa muda waliopewa baada ya kuchaguliwa na kuteuliwa katika nafasi mbalimbali.
Amesema hayo akiwa Visiwani Zanzibar alipokuwa akizungumzia hali ya Usalama kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2019 visiwani humo.
Kuhusu hali ya usalama kwa kipindi cha 2019, amesema matukio ya mauaji yamepungua kutoka 40 mwaka 2018 hadi 35 mwaka 2019 huku matukio ya udhalilishaji yakiongezeka kutoka matukio 15 mwaka 2018 mpaka matukio 35 mwaka 2019.