Serikali nchini, imesema itaendelea kuwaunga mkono Vijana wanaobuni teknolojia mbalimbali zinazosaidia katika kutatua changamoto za mazingira zinazoikabili nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo wakati akifungua Kongamano la Bunifu katika Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema, changamoto za mazingira hasa ukame unayoyakabili baadhi ya maeneo nchini pamoja na usimamizi wa taka ngumu zinakwenda kutatuliwa kupitia vijana wanaojikitika katika kununi nyenzo rafiki wa mazingira.

Wabunifu na wadau mbalimbali wakiwa katika Kongamano la Bunifu katika Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi ambalo lilifunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (hayupo pichani) jijini Dar es Salaam, Agosti, 2023.

Dkt. Jafo pia ametoa rai kwa vijana kutumia fursa ya kukusanya taka ngumu na kutengeneza bidhaa mbalimbali hatua itakayowapatia ajira na pia kusaidia katika shughuli ya utenganishaji wa taka.

“Tunaelezwa hapa, nchi yetu inazalisha mamilioni ya tani za taka ngumu kwa mwaka na kati ya hizo ni asilimia 30 tu ndizo zinaingia katika mfumo rasmi wa uchakataji hivyo teknolojia hizi vijana mlizobuni zitasaidia sana katika utunzaji wa mazingira, niwaombe muendelee kujikita katika teknojia ya recycling (urejelezaji) ya taka,” alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ubunifu na Teknolojia wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw. Gerald Kafuku alisema wanaendelea kuratibu, kuendeleza na kusaidia vijana katika teknojia.

Liverpool yakataa kumuuza Mo Salah
Aweso ataka usimamizi huduma bora za Maji bila upendeleo