Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua Mpango Mkakati wa miaka nane wa AMREF Tanzania na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kufanya ufuatiliaji ili kuhakikisha afua zilizopo katika mpango huo zinatekelezwa kwa ufanisi na kuboresha huduma za afya kwa Watanzania.

Majaliwa ameyasema hayo Septemba 15, 2023 wakati akizindua mpango huo jijini Dar Es Salaam wa kuanzia mwaka 2023 hadi 2030, ili kuelekea katika malengo ya maendeleo endelevu ya dunia 2030, unaotarajia kugharimu dola la kimarekani milioni 458 kwa miaka yote nane.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema, mpango mkakati huo utajikita katika kuboresha Afya ya msingi ikiwemo, kutekeleza afua za afya ya uzazi pamoja na afya ya mama na mtoto, afua za magonjwa yasiyoambukiza utasaidia katika kuimarisha afya na ustawi wa Watanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu amesema gharama za kutekeleza mpango mkakati huo itakuwa inaongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka 2023 itakuwa ni Dola za marekani milioni 40 ambayo itakuwa ikikua kwa asilimia 30.

Mashirika yasiyo ya Kiserikali yazingatie maadili - Majaliwa
Lugha ya Kiswahili yaimarisha udugu Tanzania, Cuba