Serikali imesema kuwa inatarajia kununua kondomu zitakazosambazwa nchi nzima bure kwa lengo la kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Neema Rusibamaila wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa kondomu.

Dkt. Rusibamaila amesema kuwa kutakuwa na mashine maalumu zitakazofungwa kwenye maeneo ya sehemu za starehe kama Baa, Nyumba za kulala wageni, Migodini na katika kumbi za burudani ili kuweza kufanikisha zoezi hilo.

“Takwimu zinaonyesha kuwa 69% ya wanawake na 77% ya wanaume wanafahamu kwamba kondomu inaweza kuzuia VVU, lakini ni 27% tu ya watu wenye wenza zaidi ya mmoja walitumia kondomu walipofanya ngono mara ya mwisho,”amesema Dkt. Rusibamaila

Hata hivyo, ameongeza kuwa Kondomu hizo zitanunuliwa kupitia fedha za Global Fund, ili kufikia malengo ya kupunguza maambukizi ya VVU ifikapo mwaka 2030.

 

 

CCM yavikaanga vyama vya upinzani
Mwashiuya: Simba SC wamenifuata nisaini