Serikali imesema kuwa haiwezi kuvumilia kuona wananchi wake wanapata shida, wanaumizana kutokana na matukio ya uchaguzi kisha wao wakae kimya bila ya kuchukua hatua yeyote kwa kuwa wao wapo kwa ajili ya kulinda usalama wao.
Hayo yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba, ambapo amesema kuwa serikali haipendi kuona wananchi wake wakinyanyasika.
“Sisi kama Jeshi la Polisi na kama Wizara ya Mambo ya Ndani hatupendi kuona wananchi wetu wanaumizana kwenye masuala ya uchaguzi na kwenye chaguzi nyingi tumeshuhudia. Mara zote huwa nasema kwamba ni aibu sana kwa nchi yenye vyama vingi vya siasa halafu wananchi wake wanafanyiana fujo pale panapotokea uchaguzi katika eneo husika,”amesema Dkt. Nchemba
Hata hivyo, Dkt. Nchemba amewataka Wabunge waliopo Bungeni kuacha tabia ya kuunganisha matukio na imani ya dini au siasa.