Serikali Nchini, itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuimarisha mifumo na miuondombinu ya mifumo ili kuboresha ufanisi wa utoaji huduma, utendaji kazi na kupunguza urasimu unaokwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Kuhudumia Wawekezaji Mahali Pamoja; Mwongozo wa Kuwasajili Watoa Huduma za Ushauri kwa Wawekezaji pamoja na Kampeni ya Uhamasishaji Uwekezaji jijini Dar es Salaam.

Amesema, “Kituo cha uwekezaji kimekuwa kikifanya maboresho mbalimbali ili kuongeza kasi ya kutoa huduma. Matokeo ya jitihada zote hizo za kuongeza ufanisi ni pamoja na kuanza kutumika kwa mfumo wa kuhudumia wawekezaji mahali pamoja (Tanzania Electronic Investment Window-TeIW).”

Aidha Waziri Mkuu ameongeza kuwa, kuanza kutumika kwa mfumo huo ni matokeo ya utekelezaji wa mpango wa maboresho ya mazingira ya biashara na uwekezaji nchini unaojumuisha maboresho ya sheria, sera na mifumo ya utendaji kazi katika kuhamasisha uwekezaji.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimeandaa mwongozo mahsusi wa kusajili Watoa Huduma za Ushauri kwa Wawekezaji ambao umeorodhesha aina za huduma zinatozotolewa na watoa huduma kwa wawekezaji, vigezo vya kuwa mtoa huduma kwa wawekezaji, utaratibu wa kuwasilisha maombi ya kuwa mtoa huduma kwa wawekezaji, mafunzo kwa watoa huduma na ufuatiliaji na tathmini ya watoa huduma hao.

Singida Fountain Gate matumaini kibao Misri
Young Africans kuweka rekodi Afrika