Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mtwara utakaogharimu Shilingi Bilioni 55.
Hayo yamesemwa mkoani Mtwara na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela ambapo amewahakikishia wananchi wa Mtwara kuwa kazi ya upanuzi mkubwa wa uwanja huo itaanza.
“Kuna mradi wa takribani shilingi Bilioni 55 kupanua Uwanja wa Ndege wa Mtwara na kazi inakwenda kuanza, pia kuna kazi za ukarabati Uwanja wa Songea na Nachingwea yote ni katika kulifungua eneo la Kusini,” amesema Mayongela
Aidha, Mayongela amesema kuwa mradi huo una lengo la kuimarisha usafiri wa anga katika maeneo ya kusini mwa Tanzania ili kuiunganisha na mikoa mingine.
Mayongela aliongeza kuwa Mradi huo utatekelezwa na mkandarasi kutoka China na tayari yupo katika eneo la mradi,
-
Mngereza aeleza alivyochangamkia mchongo wa TACIP, ‘inaongeza thamani’
-
Mbunge alalamikia malipo kidogo ya Korosho
-
Fastjet yapewa notisi ya siku 28, yatakiwa ijitafakari
Kwa upande wake Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha inazijenga na kuziboresha barabara za vijijini kupitia Taasisi ya TARURA iliyopewa jukumu la kusimamia eneo hilo.