Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amebainisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Serikali inatarajia kuleta mabehewa na vichwa vya treni ya umeme 1,400.

”Julai mwaka huu, kichwa cha treni ya umeme kitaletwa kwa majaribio kwenye SGR” amesema Msemaji wa serikali.

Hayo yamebainishwa alipokuwa akizungumzia tukio la uungwaji wa reli ya treni za Umeme, Standard Gauge Railway kuunganishwa kwa vipande vya SGR na kufanya reli hiyo kuwa moja kutoka Morogoro hadi Dar.

Uliofanyika Aprili 14, 2019 katika kijiji cha Soga mkoani Pwani na kuhudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe

Waziri Kamwele alieleza kuwa ifikapo mwezi wa saba mwaka huu, Mkandarasi wa reli hiyo ya Shirika la Reli nchini(TRC) wataleta kichwa cha treni ya umeme kwa ajili ya majaribio kwenye kipande cha reli cha Kilometa 30.

Mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge – unaendelea. Reli hiyo itaanzia bandari ya Dar es Salaam hadi mji mkuu wa Dodoma na baadaye hadi nchi za jirani za Rwanda Burundi na DR Congo.

Mradi huo umeelezwa kuwa mkubwa zaidi katika miundombinu kufanyika miaka ya hivi karibuni na manufaa yake kiuchumi kuwa makubwa si kwa Tanzania tu bali hata nchi za jirani.

Mradi huo utagharimu dola Bilioni 1.92, lakini ndio utakuwa mradi nafuu zaidi wa reli kufanyika Afrika Mashariki.

Gharama hiyo ni nusu ya ile ambayo Kenya ilitumia kujenga awamu yake ya kwanza ya reli ya hivi karibuni kutoka Mombasa hadi Nairobi.

Video: Jibu la Cardi B kuhusu kutumbuiza na NickiMinaj
Rais Tshisekedi aanza ziara ya ndani, azuru Kivu Kaskazini

Comments

comments