Serikali imesema kuwa itatimiza ahadi zake za kupandisha hadhi vituo vya Afya vya Nanyumbu na Nangurukuru vilivyopo Mkoani Mtwara kuwa na hadhi ya hospitali.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge.

Amesema kuwa ahadi za Serikali za kupandisha hadhi ya vituo hivyo vilivyopo mkoani Mtwara kuwa hospitali kamili ziko pale pale hivyo hakuna mabadiliko yoyote ambayo yamejitokeza.

“Serikali itatimiza kila kitu ambacho imekiahidi katika vituo hivyo, kwani ni muhimu sana kwa wananchi wa maeneo hayo, kinachosubiriwa ni kukamilika kwa taratibu tu ili kazi ianze,”amesema Jafo.

Hata hivyo, katika hatua nyingine Jafo ameongeza kuwa Serikali imeshawekeza vifaa vya vingi vya kitaalamu ambavyo vitawezesha zoezi zima kufanyika kwa ufasaha na haraka zaidi.

Uchaguzi TAFCA Kinondoni Juni 04
Himid Mao Kuanza Majaribio Leo