Serikali nchini, imesaini mkataba wa uzalishaji na ugawanaji mapato (PSA), kitalu cha Ruvuma – Mtwara ikiwa ni baada ya kupita kipindi cha miaka 12.
Mkataba huo, unaweka utaratibu wa Serikali kupata mapato zaidi kwa mara ya kwanza kupitia mapato ghafi (Gross), ambapo itapata asilimia 75 ikiilinganishwa na awali ilipokua ikipata asilimia 68 kushuka chini.
Mara baada ya kusaini mkataba huo, Waziri wa Nishati, January Makamba amesema, “Siku hii ni kubwa na ya Kihistoria sababu Serikali inaenda kupata asilimia 75 ya Mapato Ghafi.
Makamba ameongeza kuwa, “Hii ndo tafsiri ya win-win na kazi hii imefanywa ndani ya mwaka mmoja natoa wito kwa wawekezaji kufanya kazi kwa haraka, ili ndani ya miezi 12 hadi 18 Gesi hii ianze kutumika.