Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa ‘BMT’, imeahidi kahakikisha timu ya Taifa ya Riadha Tanzania chini ya miaka I8 na 20 inashiriki vema mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Zambia Aprill 2 hadi Mei 3, mwaka huu.

Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa BMT, Neema Msitha alipotembele kambi ya timu hiyo iliyopo kwenye Hosteli za Baraza la Maaskofu Tanzania (IEC), Kurasiní jijiní Dar es salaam.

Msitha, mbali na kupongeza mandhari na huduna kambini hapo, amesema Serikali inatambua na kufautilia kambi hiyo kwa ukaribu.

Akizungumza na wachezaji baada ya kufika kambini hapo, Msitha amesema: “Serikali ya mama Samia imeweka msisitizo katika mambo mengi ikiwemo michezo, jambo linaloleta matokeo chanya, hivyo niwahakikishie kuwa itakuwa pamoja nanyi licha ya tayari kuwa kuna mambo tayari tumeyafanya ili kuhakikisha mnakwenda kuliwakilisha vema Taifa bila ya kuwa na msongo wa mawazo.

“Hakuna ajira duniani inalipa mapema kama ile itokanayo na kipaji cha mtu, hivyo nyie kuwa hapa miongoni mwa Watanzania wengi, mtambue kuwa mna kitu, hivyo ni kazi kwenu kujituma binafsi kujiendeleza.”

Kiongozi huyo amewataka vijana hao kuzingatia mazoezi wanayopewa na makocha wao ili waende wakafanye vema katika mashindano hayo na kuwaahidi warejee na medali kwani kuna ‘sapraizi’ watakutana nayo watakaporejea.

Awali, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), William Kallaghe, alisema kambi hiyo inaundwa na wachezaji 15, makocha wawili, meneja na daktari.

ASA kuzalisha tani 4,000 za mbegu msimu wa Kilimo
JKT Tanzania: Ubingwa Championship ni suala la muda